Header Ads

Header ADS

Makamo wa Rais Sudani Kusini avuliwa madaraka

         Riek Machar amevuliwa madaraka kama kiongozi wa chama chake, wakati wapinzani wake ndani ya chama hicho wakimshtumu kutowakilisha tena maslahi yao. 
Machar, ambaye amekuwa na mchango muhimu katika mapambano ya kupigania uhuru wa Sudan Kusini, na pia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyofuatia, amevuliwa madaraka hayo kufuatia mkutano wa siku tatu wa viongozi wakuu wa chama cha SPLM/A-IO kaskazini mwa nchi hiyo. 
Tawi la kijeshi la chama hicho limesema mkuu wa utumishi Luteni Jenerali wa kwanza Simon Gatwech Dual ametangazwa kuwa kiongozi wa mpito wa vuguvugu hilo la upinzani ambalo linaongoza nchi hiyo katika serikali tete ya muungano na mahasimu wao wa zamani. 
Haijabainika wazi nini maana ya hatua hiyo ya kumuondoa Machar, ambaye amenusurika miaka mingi ya vita vya msituni, na majaribio ya mauaji pamoja na kuishi uhamishoni.


No comments

Powered by Blogger.