Header Ads

Header ADS

Bado kuna uwezekano wa shambulio la Urusi - Ukraine

 Shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine "bado lina uwezekano mkubwa wa kufanyika ", lakini garama ya kibinadamu ''itakuwa kubwa'', amesema Rais wa Marekani Joe Biden.
Katika hotuba yake ya kitaifa iliyotangazwa na televisheni kote nchini, Bw Biden alisema Marekani iko tayari kujibu kwa hatua ya haraka.
Rais huyo wa Marekani amesema kuwa Urusi sasa imerundika kiasi cha wanajeshi 150,000 kwenye mpaka wake na Ukraine.
Waziri wa ulinzi wa Urusi amesema baadhi ya wanajeshi wameondoka. Bw Biden amesema kwamba hilo halijahakikishw

[Kuondoka kwa vikosi vya Urusi] itakuwa vizuri , lakini bado hatujahakikisha hilo. Hatujahakikisha kuwa vikosi vya kijeshi vya Urusi vinarudi kwenye ngome zake za nyumbani ," rais wa Marekani alisema. "Kwa kweli, tathmini yetu inaonyesha kwamba bado wapo katika nafasi ya kutisha ."
Hotuba ya Biden inakuja saa kadhaa baada ya rais wa Urusi Vladimir Putin kusema kuwa hofu za usalama za Urusi zinapaswa kutatuliwa na kuchukuliwa kwa umakini.
Bw Putin kila mara amekuwa akikana kuwa anapanga shambulio, na alisema Urusi haitaki vita nyingine katika Ulaya. Hatahivyo hali ya wasi wasi imekuwa ikiongezeka tangu mwezi wa Disemba.


No comments

Powered by Blogger.