Header Ads

Header ADS

Kikosi cha Young Africans kimeendelea kutimua vumbi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

 Kikosi cha Young Africans kimeendelea kutimua vumbi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuichabanga Mtibwa Sugar mabao 2-0 .
Young Africans iliyokua Manungu Complex Mkoni Morogoro kama Mgeni wa Mtibwa Sugar katika mchezo huo wa Mzunguuko wa 15 wa Ligi Kuu, imepata mabao hayo kupitia kwa Saido Ntibanzonkiza na Fiston Mayele.
Ushindi huo kwa Wananchi unaendelea kuongeza ari ya ubabe katika michezo ya Ligi Kuu msimu huu, huku ukithibitisha timu hiyo kuwa na rekodi ya kipekee ya kutokufungwa tangu msimu wa 2021/22 ulipoanza.

Ushindi huo umeiwezesha Young Africans kufikisha alama 39 kwenye msimamo wa Ligi Kuu na kuwaachama Mabingwa Watetezi Simba SC wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya alama 8.


No comments

Powered by Blogger.