Header Ads

Header ADS

Kirusi cha polio chagundulika Malawi

 Shirika la afya duniani WHO limesema maafisa nchini Malawi wamegundua kisa cha maambukizi ya kirusi cha polio kinachosababisha ugonjwa wa kupooza katika mji mkuu wa nchi hiyo Lilongwe. 
Kisa hicho ni hatua nyingine ya pigo katika juhudi za kuumaliza kabisa duniani ugonjwa huo wa kupooza unaoambukiza haraka. 




Katika taarifa yake iliyotolewa leo, shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema maafisa wa Malawi wamegunduwa kirusi cha polio kwa mtoto mdogo mjini Lilongwe ikiwa ni mara ya kwanza kirusi hicho kugundulika katika bara hilo la Afrika katika kipindi cha miaka mitano. 
Ingawa ugonjwa wa kupooza umekuwa ukienea katika nchi mbalimbali za Afrika katika kipindi cha miaka ya karibuni, kuripuka maradhi hayo kulihusishwa na virusi ambavyo kimsingi vilidhibitiwa kupitia chanjo na sio kirusi hiki cha sasa. 
Katika hali ambayo sio aghalabu kutokea, kirusi hicho kinaweza kujibadilisha na kugeuka kuwa kirusi sugu chenye uwezo wa kusababisha janga na hasa katika maeneo yenye idadi ya watu ambao hawajachanjwa. 
WHO limesema vipimo vya maabara vimeonesha kirusi hicho cha polio kilichogunduliwa Malawi kina mafungamano na kile ambacho kimekuwa kikisambaa katika mkoa wa Sindh nchini Pakistan ambako ugonjwa huo wa kupooza bado haujatokomezwa.



No comments

Powered by Blogger.