Header Ads

Header ADS

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imewakuta na kesi ya kujibu Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe pamoja na wenzake watatu katika kesi inayowakabili

 Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imewakuta na kesi ya kujibu Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe pamoja na wenzake watatu katika kesi inayowakabili  namba 16 ya mwaka 2021.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Februari 18, 2022 na Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo 

Akisoma uamuzi huo leo Jaji anayesikiliza shauri hilo Jaji Tiganga ameeleza kuwa shitaka la sita lililokuwa likimkabili mshtakiwa wa kwanza pekee ambaye ni Halfan Hassan Bwire, limefutwa kutokana na waliochukua vielezo hivyo hawakufuata utaratibu.

Aidha, Jaji Tiganga amefafanua kuwa washtakiwa wote wanne wamekutwa na mashtaka matano ya kujibu na akawataka waeleze utaratibu watakaoutumia kuleta mashahidi wao.

Mawakili wa upande wa utetezi wakiongozwa na wakili Peter Kibatala wamaelza Mahakama kuwa watakuwa na mashahidi zaidi ya 20 wakiwepo washitakiwa wenyewe watakaojitetea chini ya kiapo.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa maarufu kama Adamoo na Mohamed Abdillahi Ling’wenya.

Hii ni kesi namba 16 ya mwaka 2021 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA na wenzake watatu kwa mashtaka ya uhujumu uchumi ambayo ndani yake kuna makosa ya ugaidi.

No comments

Powered by Blogger.