Header Ads

Header ADS

Polisi adakwa kwa kukutwa na Dawa za kulevya

 Polisi wa kike kutoka nchini Jamaica, amekamatwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine gramu 1,350 akiwa amezificha sehemu mbalimbali za mwili wake, wakati akijaribu kuingia nazo nchini Marekani
Polisi huyo, Shelian Cherine Allen mwenye umri wa miaka 42, amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale-Hollywood International Airport, muda mfupi baada ya kuwasili akitokea Montego Bay, Jamaica.
Kwa mujibu wa maafisa wa polisi, mwanamke huyo amekutwa na dawa hizo akiwa amezificha kwenye sehemu zake za siri, kwenye sidiria aliyokuwa amevaa huku pia akiwa amemeza takribani kete 90 tumboni mwake.
Endapo atakutwa na hatia, mwanamke huyo anaweza kuhukumiwa kifungo cha takribani miaka 40 jela.


No comments

Powered by Blogger.