Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akataa kufanyiwa vipimo vya Covid nchini Urusi
Uchunguzi huo ulihitaji itifaki ya afya ambayo haikubaliki na haiendani na ratiba ya kiongozi huyo wa Ufaransa, chanzo cha Ufaransa kiliambia BBC.
Hatua hiyo nafuatia ripoti kwamba Bw Macron alikataa kipimo cha PCR kwa hofu kwamba Warusi wangepata DNA yake.
Viongozi hao baadaye walifanya mkutano huku wakiwa wamekaa mbali kijamii siku ya Jumatatu.
Hawakusaliamia kwa mikono na kukaa na meza yenye urefu wa mita nne kati yao, huku waangalizi wakishangaa iwapo Bw Putin alikuwa akiitumia njia hiyo kutuma ujumbe wa kidiplomasia.
Lakini vyanzo vya kidiplomasia vya Ufaransa viliiambia Reuters kwamba Bw Macron alikuwa ameambiwa achague kati ya kukubali vipimo vya PCR vya Urusi ili kuwa karibu na Putin au kutii sheria kali za kukaa mbalimbali.
Tulijua vizuri kwamba hatua hiyo ilimaanisha kwamba hakutakuwa na kusalimiana kwa mkono katika meza hiyo ndefu. Lakini hatukubali waweze kupata DNA ya rais, mmoja ya vyanzo hivyo aliambia Reuters.
Chanzo hicho hakikuelezea jinsi huduma hiyo ya ujasusi wa Urusi ingetumia DNA ya bwana Macron.
Chanzo hicho katika Jumba la Elysee aliambia BBC: Masharti yaliowekewa mkutano huo kufanyika bila ya kuwepo kwa masharti ya corona itifaki ya kiafya ambayo isingekubalika na ratiba ya rais.
Kremlin ilihiboitisha kwamba bwana Macron alikaa mbali na kionhozi huyo wa Urusi kwasababu alikataa kufanyiwa vipimo Urusi.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema kwamba Urusi inaelewa uamuzi huo huo wa Ufaransa na haikuathiri mazungumzo.
Bwana Macron alifanya vipimo vya PCR kabla ya ya kuondoka Ufaransa na daktari wake alifanya vipimo walipofika Mosvow , chanzo chengine cha kidiplomasia kiliambia Reuters.
Warusi walituambia kwamba Putin alihitajika kufauta sheria kali za kiafya , chanzo cha pili kilisema.
No comments
Post a Comment