Header Ads

Header ADS

Wafanyakazi Azam TV wapata ajali

 Wafanyakazi 12 wa Azam Media Limited (AML) wamepata ajali katika Mlima Kitonga, mkoani Iringa, baada ya gari lao kusukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharura. 
Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022. Majeruhi wanaendelea na matibabu kutoka kwa matabibu wa Mkoa wa Iringa.

Wafanyakazi hao walikuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC.
Uongozi wa Azam Media Limited umethitisha kutokea kwa ajali hiyo na umewashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.


No comments

Powered by Blogger.