UN yaitaka urusi kusitisha vita nchini ukraine
Geneva,Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura azimio jipya ambalo iwapo litaidhinishwa, litaitaka Urusi kusitisha vita vyake nchini Ukraine. Kura hiyo inakuja baada ya nchi 141 wanachama kuidhinisha azimio la awali mnamo Machi 2, ambalo pia linaitaka Urusi kusitisha matumizi ya dhidi ya ukraine
Katika kura hiyo, nchi tano ikiwemo Urusi, ilipiga kura ya Hapana dhidi ya azimio hilo wakati nchi 35 hazikushiriki kura hiyo. Azimio hilo halikuwa na ulazima wa kisheria kutekelezwa, bali ni kuonyesha kutoungwa mkono kwa Urusi duniani, na halikuonekana kuwa na ushawishi wowote wa kuizuia Urusi kuendelea na vita.
Jana Jumatano, Ukraine iliwasilisha azimio jipya mbele ya kikao kingine cha dharura cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. Rasimu ya azimio hilo iliyoonekana na shirika la habari la AFP, linaungwa mkono na nchi 88 na awali lilikuwa limetayarishwa na Ufaransa na Mexico.

No comments
Post a Comment