Mubunge wa kawe atema cheche bungeni
Mbunge wa Kawe (CCM), Askofu Josephat Gwajima amesema kama Taifa halitakuwa na maono itasababisha kila Rais anayeingia madarakani kuanza chake na matokeo yake ipo siku Tanzania itapata kiongozi wa ajabu na hivyo kuangukia pua.
Askofu Gwajima ameyasema hayo Jumatatu Aprili 11, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Gwajima amesema kuna sababu ambayo inaifanya Tanzania ibaki ilipo kwa muda mrefu.
Amesema Tanzania inahitiji dira ama ajenda ya au maono ama mwelekeo wa Taifa.
Amesema yeye amewahi kufika zaidi ya mataifa 143 na kwamba hajafika katika mataifa 50 tu duniani lakini kwa mshangao mataifa ya Afrika yote yanaasili ya kufanana, yana matatizo ya kufanana na yako nyuma kwa aina ya kufanana.
Gwajima amesema amegundua kuwa mataifa hayo hayana maono ya muda mrefu ambayo yanalifanya Taifa liongozwe (guided) katika mamlaka.
Ametoa mfano United Arab Emirate wanampango wa 2050 hadi 2117 kuhamishia makazi ya kwanza katika sahari ya Mars.
Pia amesema Muungano huo unampango wa kuwa nchi ya kwanza kati ya nchi 10 duniani zenye hifadhi kubwa ya chakula.
Mbunge huyo amesema hakuna nchi iliyoendelea duniani bila kuwa na mpango wa muda mrefu na kwamba kusipokuwa na mpango wa maendeleo wa muda mrefu kasi Tanzania haitaenda kama inavyotakiwa.
Askofu Gwajima amesema Katiba ya nchi ibara ya 63 kifungu cha 3 C inaliruhusu Bunge kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu ama mfupi unaokusudiwa kutekelezwa na kutunga sheria ya kusimamia mpango huo.
Amesema kuna hatari itakayolipata Taifa siku zijazo na ndio maana watu wamekuwa wakisema wanahitaji Rais mwenye maono na kwamba hayo yote yanatokea kwasababu nchi haina maono.
“Tunahitaji maono ili kila Rais anayeingia madarakani afuate maono tuliojiwekea ipo siku kama tutaruhusu kila anayeingia madarakani aongozwe na kichwa chake kuna siku tutapata Rais wa ajabu tutadondokea pua na hatutaamini macho yetu,”amesema.
Amesema kuwa baada ya vita vya pili nchi za Ulaya zilifirisika ambapo Marekani walianzisha mpango maalumu wa kuzisaidia nchi za ulaya magharibi 17 ambazo zilifilisika kabisa.
Amesema Marekani iliwapa dola za marekani bilioni 13 ambazo sasa hivi ni sawa na dola za marekani 115 na kuwataka kutengeneza mipango yao ya muda mrefu.
Askofu Gwajima amesema ni vyema mitaala ya shule, ilani zote za CCM na watoto waweze kujifunza na kuiona Tanzania na kwamba vinginevyo tutapoteza muda mwingi sana kwa kuzunguka palepale na kufanya mambo yale yale.
Amesema awamu zilizotangulia zilifanya vizuri sana lakini hazikuendelea kila awamu zilikuja na mambo yake hazikuendelea zilipoishia zilizomtangulia.
“Tumekuwa na Mwalimu Nyerere (Julius) aliendelea kwa namna yake, akaja Mwinyi (Alli Hassan) ameenda kwa namna yake lakini alipoishia Mwinyi, Mheshimiwa Mkapa (Benjamin Mkapa) hajaendelea pale, alipoishia Mkapa Kikwete (Jakaya Kikwete) hajaendelea pale Magufuli (John Magufuli).
Tunakuwa na kila Rais anaingia madarakani anaanza chake na matokeo yake tutapata Rais wa ajabu tutaangukia pua hujawahi kuona.”
No comments
Post a Comment