Header Ads

Header ADS

Ukraine yamtia mbaroni Viktor Medvedchuk,

 Kyiv Shirika la ujasusi la Ukraine SBU limemkamata mwanasiasa wa upinzani nchini humo Viktor Medvedchuk, ambaye anaunga mkono Urusi na anatajwa kuwa mshirika wa karibu wa rais Vladimir Putin. 
Kigogo huyo mwenye umri wa miaka 67 anachukuliwa kuwa mtu muhimu katika mzozo kati ya Moscow na Kyiv kwa miaka mingi. Alikamatwa Mei mwaka jana na kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani lakini alitoroka kabla ya Urusi kuanza uvamizi. 

Wakati huohuo, vikosi vya Urusi vimezidisha kampeni ya kuudhibiti mji wa Mariupol, kama sehemu ya mashambulizi makali ambayo yametabiliwa katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine. 
Rais Vladimir Putin ameapa kuendeleza mashambulizi mpaka pale malengo yake yatakapotimia na kusisitiza kuwa kampeni inaendelea kama ilivyopangwa licha ya kupata upinzani kutoka Kyiv.


No comments

Powered by Blogger.