Ahmed Ally aipiga kijembe Young Africans
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba Ahmed Ally ameipiga kijembe Young Africans kwa kuitaka kuondoa kitu kilichofukiwa katikati ya la Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya mchezo wa jana Jumatatu (Mei 09) dhidi ya Tanzania Prisons.
Kumekua na mkanganyiko wa nani alifukia kitu hicho katikati ya eneo la kuchezea, kufuatia picha zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuonyesha wachezaji wa Tanzania Prisons wakifanya dua ya pamoja, lakini baadae beki wa kulia wa Young Africans Djuma Shaban alikwenda eneo hilo na kuonekana akifanya jambo fulani.
Ahmed Ally amewaomba Young Africans kukiondoa kitu hicho ili kutoa nafasi kwa timu yao kucheza kwa amani kesho Jumatano (Mei 11) katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.
No comments
Post a Comment