BALOZI WA TANZANIA NCHINI ETHIOPIA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO UNECA
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Kamisheni Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA), Mhe. Innocent Eugene Shiyo, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe.Dkt. Vera Songwe, Katibu Mtendaji wa Kamisheni Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA).
Wakati wa hafla hiyo, Mhe. Dkt. Vera Songwe alimpongeza Balozi Shiyo kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA) yenye Makao Ma
kuu Jijini Addis Ababa, Ethiopia na amemkaribisha na kumtakia heri katika utekelezaji wa majukumu yake.
Wakati wa mazungumzo yao, Balozi Shiyo na Dkt. Vera
Songwe wamekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na
UNECA katika masuala ya kipaumbele ikiwemo utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo
Endelevu, Mpango wa Maendeleo wa Afrika wa Agenda 2063 na juhudi za kukwamua uchumi
dhidi ya madhara ya UVIKO-19.
Dkt, Vera Songwe ameeleza utayari wa UNECA kuisadia
Tanzania kujenga na kuimarisha uwezo katika mikakati ya kukuza sekta za
utalii,afya, kilimo,sekta binafsi, ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa Mkataba
wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA), mapambano dhidi ya Mabadiliko ya
Tabianchi na uwezeshaji Wanawake kwenye matumizi ya Teknolojia.
Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika
ilianzishwa mwaka 1958 kwa ajili ya kukuza maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii
katika nchi za Afrika, kukuza Mtangamano wa Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa
kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.
No comments
Post a Comment