Header Ads

Header ADS

Diwani aliyetoweka akutwa kwa mwanamke Tabata


Jeshi la polisi Kanda maalum Dar es salaam limesema Diwani wa Kata ya Kawe Mutta Rwakatare aliyetoweka tangu mwezi wa pili amekutwa nyumbani kwa mwanamke mmoja Tabata Dar es salaam

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro

Mwanamke huyo Ashura Ally ameliambia jeshi la Polisi kuwa Diwani huyo alifika nyumbani kwake akiwa katika hali ya ulevi

Hivi karibuni  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni alinukuliwa akieleza kuwa  Diwani wa Kata ya Kawe Mutta Rwakatare, hajulikani alipo tangu mwezi wa pili mwaka 2022.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limesema baada ya taarifa hizo walifanya uchjunguzi wao na ufuatiliaji wa taarifa hizo na kufanikiwa kumpata diwani huyo tarehe 23/05/2022 akiwa kwenye nyumba ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Ashura Ally Matitu, miaka 43, Mzaramo mkazi wa Tabata darajani ambaye alidai kuwa Diwani huyo ni rafiki yake wa siku nyingi

Mwanamke huyo aliwaeleza Polisi kuwa diwani huyo alifika nyumbani kwake tarehe 19/05/2022 huku akiwa katika hali ya ulevi uliopindukia.

Taarifa ya polisi imeeleza kuwa Kutokana na mazingira ya ulevi ambayo Diwani huyo amekutwa nayo na maombi yaliyotolewa na ndugu zake kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya matibabu, ndugu pia walitoa kumbukumbu za nyuma, mwenendo na tabia za Diwani huyo hivyo Jeshi la Polisi limemkabidhi diwani huyo kwa ndugu zake kwa matibabu na tiba zaidi za kisaikolojia.




No comments

Powered by Blogger.