Fursa kwa Watanzania : nafasi za kazi za Makarani na Wasimamizi wa Sensa 2022
Serikali imetoa onyo kwa baadhi ya watu na makundi, yenye nia mbaya kwa zoezi la sensa ambao wamekuwa wakitoa matangazo ya ajira za sensa kwa nia ya kuwatapeli wananchi wanaohitaji kushiriki katika zoezi hilo.
Mhe. Simbachawene alisema kwamba mchakato wa ajira za makarani na wasimamizi kuanzia Mei 05 hadi Mei 19,2022 ambao utahusisha ngazi zote za kiutawala kuhakikisha wanapatikana makarani na wasimamizi wenye sifa stahiki.
==>>BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI
Vilevile Mhe. Simbachawene aliwahimiza watanzania wote wenye sifa ambao wangependa kuomba nafasi za ajira hizo kufuata utaratibu uliowekwa kwa ukamilifu ili kuomba nafasi hizo.
“Kazi za kufanya pamoja na sifa za mwombaji zimebainishwa katika Tangazo la Ajira za Muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.Hakutakuwa na maombi yatakayofanyiwa kazi zaidi ya yale yatakayofuata utaratibu uliowekwa mtandaoni,”alifafanua Mhe. Simbachawene.
Kuhusu namna ya kufanya maombi hayo alibainisha kwamba waombaji watatakiwa kutuma maombi yao kupitia mtandao (online) ambao hautahusisha malipo yoyote kwa mwombaji wa ajira.
==>> BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI
” Mfumo wa kuomba ajira hizi kupitia mtandao unapatikana kupitia tovuti zifuatazo;www.pmo.go.tz, www.tamisemi.go.tz, www.nbs.go.tz kwa Tanzania Bara na www.ompr.go.tz, https://www.tamisemim.go.tz au www.ocgs.go.tz kwa wale wanaoomba Tanzania Zanzibar,”Alieleza.
Aidha alihitimisha kuwa mchakato wa kuchambua maombi ya kazi pamoja na usaili utasimamiwa na Kamati maalum itakayoundwa katika ngazi ya kila Wilaya na usaili utafanyika katika ngazi ya kata kwa nafasi za makarani na wasimamizi wa maudhui na katika ngazi ya Wilaya kwa Wasimamizi wa TEHAMA,”alihitimisha Mhe. Simbachawene.
___________
1. Kusoma vigezo na masharti ya kazi <<bonyeza hapa.>>
2. Kujaza fomu ya maombi ya kazi za sensa <<bonyeza hapa>>
3. Ingia kwenye mfumo kukamilisha usajili(Kubadilisha taarifa na kupandisha fomu Na. 1 ya maombi ya kazi za sensa ILIYOSAINIWA)<<bonyeza hapa>>
No comments
Post a Comment