Naibu Waziri Kundo: Wadau wa habari tumieni hii fursa
Wadau wa sekta ya Habari na Mawasiliano nchini wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa maafisa uhusiano na wadau wa sekta hiyo kutoka mataifa mbalimbali, kuimarisha mfumo wa utoaji habari na mawasiliano katika maeneo yao ya kazi.
Amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini, ni fursa kwa watanzania na utazidi kufungua milango zaidi kwa wawekezaji kwenye sekta ya habari na mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa habari kutoka kwa maafisa uhusiano na mawasiliano nchini.
Mkutano huo mkuu wa 33 wa maafisa uhusiano na mawasiliano Afrika umelenga kujadili changamoto mbalimbali katika sekta hiyo na una washiriki kutoka zaidi ya mataifa ishirini barani Afrika.
No comments
Post a Comment