Rais Ebrahim wa Iran ameonya kuwa Iran italipiza kisasi kufuatia kuuwawa kwa kanali Sayyad Khodai wa kikosi cha ulinzi wa mapinduzi cha Jeshi la Iran, ambae kifo chake kilitokana na kupigwa risasi mjini Tehran.


Iran inaliunganisha tukio hilo kuwa sawa na kiburi cha mataifa ya kigeni, neno ambalo taifa hilo la Kiislamu linaunganishwa na hasimu wake mkubwa Marekani na washirika wake likiwemo Israel.


Jumapili washambuliaji waliokuwa kwenye pikipiki walimuua kwa kumpiga risasi tano Kanali Sayyad wakati alipokuwa ameketi kwenye gari lake nje ya nyumba yake huko Tehran.