Kijaji Awaomba Wawekezaji Wa Malasia Kuwekeza Katika Mafuta Ya Kula
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji,(kushoto), akizungumza na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji 10 kutoka nchini Malaysia, Hong kong, Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Jijini Dar es salaam, lengo ikiwa kujadili fursa mbalimbali zilizopo nchini hususani katika sekta ya Madini, mafuta, gesi, na biashara, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Perfect Hexagon Ltd, Sim Tze Jye, na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Link-value Lamar Resources Ltd, Shurk Albarik.
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk ASHATU KIJAJI, amewaomba wazekezaji wa Malasia wafikikirie kuwekeza katika uzalishaji wa mafuta ya kula kwa sababu Tanzania ina upungufu mkubwa wa mafuta ya aina hiyo na inalazimika kuyaagiza kutoka nje.
Akizungumza na kundi la wawekezaji Jijini hapa katika makako makuu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Waziri Kijaji amesema Tanzania ina nia thabitil ya kujitegemea katika uzalishaji wa mafuta ya kula kwa kuwa ina ardhi ya kutosha kulima mazao ya mafuta kama alizeti, machikichi, karanga na ufuta.
Takwimu za mwaka jana, zinaonyesha mahitaji ya Tanzania yalikuwa tani 570,000 na uzalishaji ulikuwa tani 250,000 ambapo zaidi ya tani 360,000 zinaagizwa nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya ndani ya nchini.
“Malasia ina sifa nzuri ya uzalishaji wa mafuta nchini mwenu. Kwa hiyo nawaomba wawekezaji wa Malesia waje wawekeze katika eneo hili hapa nchini,” ameliambia kundi la wawekezaji hao amabo wengi wametoka Malesia na wengine wametoka Visiwa vya Shelisheli, Hong Kong, Falme za Kiarabu na Poland.
Kadhalika waziri amewaaomba wawekeza wafikirie kutumia fursa za uwekezaji zilizomo katika bandari za Tanzania na kuwaomba wawekeze katika Bandari changa ya Bagamoyo ili kuipunguzia mzigo unaobebwa ba Bandari ya Dar es Salaam ambayo kwa sasa inategemewa katika uingizaji na usafirishaji bidhaa nje ya Tanzania. Amewaomba wafikirie kuwekeza katika bandari za Tanga na Mtwara.
Waziri kijaji amewakabidhi wageni hao kitabu cha muongozo kinaochoainisha fursa za uwekezaji nchini na kuwaomba wazipitie na kuchagua maeneo yatakayowafaa wao kwa uwekezaji.
Waziri Kijaji aliainisha mafanikio yaliyopatikana baada ya nchi kufungua fursa za uwekezaji,na kueleza kuwa tayari serikali imesaini mkataba wa uwekezaji na Marekani. Amesema kutokana na mkataba huo inatarajiwa miradi kadhaa itatekelezwa na kuibua ajira kwa Watanzania 60,000. Amegusia pia mkataba kati ya Tanzania na Dubai ambao miradi yake inatarajiwa kuibua ajira 500,000.
Ameongeza kuwa kutokana na jitihada ya sasa ya serikali, uwekezaji unatarajiwa kutengeneza ajira milioni nane.
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhani Dau, amesema wapo katika hatua za mwisho za mazungumzo na kampuni Access Logistic ambayo ni kampuni ya tatu kwa ukubwa duniani ili iwekeze Tanzania na kuongeza kasi ya biashara kati ya Tanzania na majirani wake.
No comments
Post a Comment