Header Ads

Header ADS

Madiwani wataka waliokwamisha ujenzi wa masoko kigoma ujiji kuadhibiwa

Mkuu wa wilaya Kigoma Ester Mahawe akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la manispaa ya Kigoma Ujiji kilichotoa azimio la kuendelea kwa ujenzi wa masoko ya Kigoma na Mwanga ambayo viongozi wachache wa masoko wanazuia ujenzi huo kwa maslahi yao.

Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Baraka Naibuha Lupoli (katikati) akizungumza kwenye kikao cha baraza la manispaa hiyo akitoa maazimio kuhusu Sakata la baadhi ya viongozi wa masoko kuzuia ujenzi wa masoko ya Kigoma na Mwanga mjini Kigoma.
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Kigoma Ujiji wakiwa katika kikao cha baraza hilo.
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Kigoma Ujiji wakiwa katika kikao cha baraza hilo.

Baraza la madiwani katika halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji limeazimia kwa kauli moja kuendelea na mpango wa ujenzi kwa ajili ya maboresho makubwa ya masoko ya Kigoma na Mwanga yaliyopo manispaa ya Kigoma Ujiji huku wakitaka kuchukulia hatua kwa viongozi wa wafanyabiashara wanaokwamisha mpango huo.

Diwani wa kata ya Rusimbi,Bakari Songoro akiwasilisha ajenda maalum ya kujadili ujenzi wa masoko hayo kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Kigoma ujiji alisema kuwa ni jambo baya linalofanywa na viongozi hao wa masoko kuzuia mpango wa maendeleo wa ujenzi wa masoko hayo.

Songorio alisema kuwa kipindi cha nyuma mpango wa ujenzi ulikwama kwa sababu ya siasa kuwepo kwa idadi kubwa ya madiwani wa upinzani lakini leo baraza lina madiani 18 wa kata wa CCM na upinzani mmoja ikiwa na diwani mmoja wa kata yanakuja masuala ya kuzuia mipango ya maendeleo yanayosababishwa na viongozi ndani ya chama hicho.

No comments

Powered by Blogger.