Spika azungumzia hatma ya wabunge wa 19 CHADEMA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKt.Tulia Ackson amesema kwa sasa hawezi kutamka kuhusu viti 19 vya wabunge wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliofukuzwa uanachama vipo wazi, kwa kuwa suala hilo lipo mahakamani.
DKt. Tulia ameliambia bunge jijini Dodoma kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki ni mahakama.
Amesema kwa kuwa tayari alipokea barua kutoka kwa wabunge hao 19 wakimtaarifu kuwa tayari wamefungua shauri mahakamani kupinga kufukuzwa uanachama, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama na badala yake linalazimika kusubiri hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi wake.
Spika amesema Alipokea Barua za Wabunge hao zikieleza kuwa Maamuzi hayo si halali, ni kinyume, hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza na kujitetea
Wabunge hao wamefungua Rufaa Mahakamani ya Kupinga Maamuzi hayo
Afisa wa Chadema alitumwa kupeleka Barua kwa Spika wa Bunge na kisha kuambiwa asubiri lakini alipokea simu kutoka kwa Viongozi wa Chadema wakimtaka aondoke eneo hilo na hivyo watafanya utaratibu mwingine wa kuituma Barua hiyo.
“Ninalazimika kutotangaza kwamba nafasi 19 za Wabunge wa Viti maalum wa Chadema hazitabaki wazi mpaka pale mahakama itakapotoa maamuzi, Kama kutakuwa na swali lolote Msemaji wa Mwisho wa jambo hii ni Spika wa Bunge na si yeyote” Spika wa Bunge Dkt. Tulia
Tarehe 12 mwezi huu Baraza Kuu la CHADEMA lilitupilia mbali rufaa ya wabunge hao ambao walikuwa wakipinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho, na hivyo kumlazimu Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwasilisha barua kwa Spika kumtaarifu kuhusu jambo hilo ili aendelee na taratibu nyingine.
No comments
Post a Comment