Header Ads

Header ADS

vikundi 31kunufaika na mkopo wa milioni 146 manispaa ya bukoba.

Mgeni Rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Mhe. Godson Gypson akizungumza wakati wa Semina Elekezi kwa Vikundi 31 Kutoka Kata 14 za  Manispaa ya Bukoba vitakavyopokea Mkopo, wakati alipokutana na Vikundi hivyo kwenye Ukumbi wa St. Theresa

Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii ipo mbioni kutoa Mkopo wa jumla ya Shilingi Milioni 146 kwa Vikundi 31 kwa kuanzia, vikiwemo  Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.

Akiongea na Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Mei 12, 2022 wakati wa Semina elekezi  iliyofanyika kwenye Ukumbi wa St. Theresa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Dkt. Mustapha Waziri  amesema kuwa Manispaa Imejipanga Kutoa Mkopo ambao hauna Riba kwa Vikundi hivyo.

Dkt. Waziri Amesema kuwa katika Mkopo huo Jumla ya Shilingi Milioni 146 zitatolewa kwa vikundi hivyo huku vikundi vya wanawake vikichukua Kiasi cha Shilingi Milioni 132, Vijana Milioni 12 na Vikundi vya Walemavu vikichukua Milioni 2    na kuwataka watakao chukua Mikopo hiyo Kurejesha kwa wakati ili na wengine waweze kuchukua.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii ya  Manispaa ya Bukoba Bw.Chinchibera Wachonke Amesema   Vipo vikundi ambavyo Vimekua vikichukua Mikopo na Kushindwa kurejesha Mikopo hiyo kwa Wakati suala ambalo limekuwa likiwanyima Watu Wengine fursa ya Kupata Mikopo Hiyo kwa Wakati.

Naye Mgeni Rasmi katika Semina hiyo Mstahiki Meya wa Manisipaa hiyo  Mhe. Godson Gypson  Amesema Manisipaa ya Bukoba Imekua Ikitoa Pesa kwa ajili ya Vikundi mbalimbali na Kumuagiza Afisa Maendeleo ya Jamii Kutoa Mkopo kulingana na waombaji walivyoomba Mikopo hiyo.

Mstahiki Meya Godson ameongeza kuwa Manispaa ya Bukoba imejipanga Kutoa Elimu kwa wale ambao watakuwa wamechukua Mkopo Huo, ikiwa Vikundi 31  ni kwa Kuanzia lakini Vikundi vyote vitafikiwa kwani Serikali chini ya Rais Samia na kwa Juhudi za Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Stephen Byabato, kilio Cha Vikundi kimesikika na lilikuwa Ni suala la muda tu.

Awali Naibu Meya Hajat Mwajabu Galiatano amevikumbusha Vikundi hivyo kutotoa hela yoyote, kwa mtumishi yeyote wa Idara yeyote, kwani Mikopo hiyo ni haki yao, ambapo kipindi Cha nyuma kulikuwepo na kasumba ya kutoa Kiasi Cha pesa ya mkopo na kuwapa Baadhi ya watumishi Kama shukrani.



Naibu Meya wa Manispaa ya Bukoba Hajat Mwajabu Galiatano akizungumza na Vikundi 31 vitakavyopokea Mkopo, wakati wa Semina elekezi iliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

Ndg. Siraji Kisaka Meneja wa NSSF Kagera, akitoa Somo juu ya Vikundi kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakati wa Semina Elekezi kwa Vikundi 31 vya Manispaa ya Bukoba vitakavyopokea Mkopo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Bukoba Chinchibera Wanchoke akizungumza wakati wa Semina Elekezi kwa Vikundi vya Wajasiriamali Vitakavyotarajia kupokea Mikopo.

Sehemu ya Wawezeshwaji wa Semina na Vikundi vya Mikopo wakiendelea kufuatilia Matukio na Mada mbalimbali Ukumbini

No comments

Powered by Blogger.