Wajumbe bodi ya tume ya taifa ya umwagiliaji watakiwa kutumia taaluma zao kusimamia na kuishauri manejimenti ya tume
Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe amewataka wajumbe wa bodi ya tume ya taifa ya umwagiliaji kutumia taaluma zao na uzoefu walionao kazini kuisimamia na kuishauri Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kutekeleza majukumu yake.
Mhe, BASHE amesema Wizara yake itazitumia nafasi 800 zilizotolewa na Serikali kuajiri wahandisi 143 wa Umwagiliaji watakao huduma katika Ofisi za Wilaya zitakazofunguliwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika Mwaka wa fedha 2022/2023 ambao majukumu yao pamoja na mambo mengine ni kusimamia skimu za Umwagiliaji.
“Tunafungua Ofisi kila Wilaya ili tuweze kusimamia kikamilifu Skimu tunazojenga,tumekuwa tukijenga Skimu za Umwagiliaji alafu tunaacha zinasimamiwa na Chama cha Ushirika tukitaraji kinasimamia vizuri, wanalima wao, wanavuna wao Banio likiharibika wanakuja Wizarani kuomba fedha za kujenga Banio”
Aidha ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuweka Wasimamizi katika skimu zote 1,097,000 nchi nzima ambazo serikali imewekeza kwa kujenga Miundombinu kwa lengo la kusimamia zoezi la ukusanyaji wa ada na tozo za Umwagiliaji kwa mujibu wa Sheria.
“Kwa mujibu wa takwimu, tunapoteza zaidi ya shilingi Bilioni miamoja kila Mwaka kwa kushindwa kukusanya ada na tozo fedha ambazo zingesaidia kutunisha mfuko wa Umwagiliaji na kuwezesha Tume kukopa Mabilioni ya fedha kwaajili ya kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya Umwagiliaji”(megar project)
Akizungumza kwa niaba ya Bodi, Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Prof. Henry Mahoo amewataka Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufanya kazi kwa kujituma ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.
“Tutatumia mbinu zozote kuhakikisha haya malengo yanafikiwa”
Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa ameahidi kuisimamia Taasisi anayoiongoza kwa weledi kufikia matarajio ya wananchi hususani katika Kilimo cha Umwagiliaji.

Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Kilimo, Wajumbe wa bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.(Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wa saba kutoka kushoto.
Kulia kwa Mhe. Waziri Bashe ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Prof. Henry Mahoo, na kushoto kwa Waziri Mhe, Bashe ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Raymond Mndolwa.)
Wajumbe wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao cha pamoja na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe jijini Dodoma.
No comments
Post a Comment