Header Ads

Header ADS

Watu 50 wameokolewa kutoka kiwanda cha chuma cha Azovstal

      Makumi ya watu wameokolewa kutoka kiwanda cha chuma kilichozingirwa ambapo wapiganaji wa Ukraine mjini Mariupol wamekuwa wakipambana kuzuia vikosi vya Urusi kuchukua udhibiti kamili wa mji huo muhimu wa kimkakati. 

Maafisa wa Urusi na Ukraine wamesema watu 50 wameokolewa kutoka kiwanda cha chuma cha Azovstal na kukabidhiwa kwa wawakilishi wa Umoja wa Mataia na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu. Jeshi la Urusi limesema, 11 kati ya waliookolewa ni watoto.

Maafisa wa Urusi na Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk wamesema zoezi la uokoaji litaendelea tena leo Jumamosi. Watu hao waliookolewa wanajumuisha wengine wapatao 500 waliokolewa kutoka mji wa Mariupol katika siku za hivi karibuni. Kulingana na makisio ya Urusi, takriban wapiganaji 2,000 wa Ukraine, wamejificha kwenye mashimo ya chini kwa chini karibu na kiwanda cha chuma cha Azovstal, na kwamba wamekataa miito ya kujisalimisha.




No comments

Powered by Blogger.