Header Ads

Header ADS

Ajinyonga baada ya kujifungua mtoto mwenye ulemavu

NJOMBE


Mwanamke mmoja mkazi wa Njombe, amejinyonga baaada ya kujifungua mtoto mwenye ulemavu. 

Kamanda wa Polisi mkoani humo Khamis Issah, amethibitisha hilo huku akiwasihi wanawake kuwa na huruma na watoto na kuhoji kama mzazi amejinyonga mtoto aliyemuacha atalelewa na nani.

Kamanda Issah ameongeza kuwa kama kuna mtu ana mpango wa kujinyonga basi haina haja ya yeye kushika ujauzito na kisha kujinyonga na kuacha mtoto, na kuwasihi wazazi kujilinda kwa ajili ya watoto wao.


"Wewe unayejinyonga na una watoto, unajinyonga kwa sababu gani, watoto bado wadogo watamtegemea nani, kama wewe una mawazo ya kujinyonga basi usiwatafute hao watoto wewe ujinyonge peke yako, kama wewe usingewatafuta wasingekuwa na wazazi," amesema ACP Issah ajinyonga

No comments

Powered by Blogger.