Aliyewatumia wanafunzi wa darasa la sita kufukua kaburi akamatwa
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Tanda Thadeo ambaye ni mkazi wa Sumbawanga mkoani Rukwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuwatumia wanafunzi wa Darasa la sita shule ya msingi Kasisiwe iliyopo Manispaa ya Sumbawanga kushiriki zoezi la kufukua kaburi la mtoto ili afufuliwe na baba yake kwa kuwalipa shilingi elfu kumi.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Rukwa ACP
Theopita Mallya amethibitisha kuwa jeshi hilo linamshikilia Tanda Thadeo mwenye
miaka 30 mkazi wa kitongoji cha Kasisiwe kilichopo manispaa ya Sumbawanga kwa
tuhuma za kuwatumia wanafunzi hao kwa madai ya kumfufua mwanae hali ambayo
imempelekea Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Rukwa kuitembelea shule hiyo na
kutoa elimu kwa wanafunzi ya kutambua matendo ya kihalifu.
Hata hivyo Marry Kway ambaye ni kamanda wa
Jeshi la Polisi wilaya ya Sumbawanga naye alikuwepo kwa ajili ya kutoa somo la
ukatili wa kijinsia na namna ya kuripoti matukio ya kiharifu kwa wanafunzi wa
shule hiyo ili kupunguza vitendo vya uvunjifu wa amani kwa jamii.
No comments
Post a Comment