Familia iliyogoma kaburi kuondolewa katikati ya barabara yakubali yaishe
Familia ya Saguda Madako, huko mkoani Simiyu imetekeleza agizo la kuondoa kaburi katikati ya barabara huku wakikubali kulipwa fidia ya shilingi laki tano na serikali.
Ikumbukwe
ni wiki moja imepita mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila kuagiza
kuondolewa kwa Kaburi lililokuwa katikati ya Barabara ya Nkindwabiye-Halawa.
Familia
hiyo iligoma kuondoa kaburi la Habi Lupigila, kwa madai kuwa hadi walipwe kiasi
cha shilingi milioni 30 na kwamba kaburi hilo lilikuwepo eneo hilo tangu mwaka
1975.
Wakizungumza
na mara baada ya kuondoa kaburi hilo baadhi ya ndugu wa marehemu wamesema
kaburi hili lilikuwa limejengwa eneo hilo ambalo hapakuwepo na barabara bali
ilikuwa sehemu ya barabara.
‘’Tulikuwa
tumejenga hapa, tukahama kwenda Matongo, wakati tunajenga hapakuwa na barabara
bali lilikuwepo zizi na baadae lilipita barabara, changamoto ni hii ya
kuhamisha kwenda kuanza mazishi upya’’’ anasema Susan Mayenga na kuongeza.
‘’Serikali tunaomba ibadilishe sheria kwa ajili ya kulipa fidia, hili tatizo
siyo kwetu tu linaweza kutokea kwa wengine, serikali ibadilishe utaratibu wa
fidia….kuna gharama za mazishi, usafiri kwa sababu ni msiba mwingine’’ anasema.
Saguda
Madako Mayenga anasema mama yake mzazi alifariki tangu mwaka 1975 na kuzikwa
katika kijiji cha Nkindwabiye, ambapo kwa sasa limepita barabara linalotoka
Byuna-Nkindwabiye hadi Halawa.
Anasema
fidia ya shilingi laki tano ambayo wamepatiwa na serikali haitoshi kwa sababu
wanahamisha kaburi na kwenda kufanya mazishi upya huku akiiomba kurekebisha
sheria ya fidia ili iweze kukidhi mahitaji.
Anaeleza kuwa familia hiyo ilikuwa haijagoma kuhamisha kaburi hilo, bali barabara ilikuwa imelifuata kaburi kwa sababu miaka ya nyuma hapakuwepo na barabara katika eneo hilo.
‘’Tuliiomba
serikali ituwezeshe kutoa kaburi, lakini hatukuweza kuelewana, sasa tumekubali
tuhamishe, japokuwa laki tano haitoshi kwa sababu tutanunua jeneza, usafiri
pamoja na chakula’’ anasema Madako akiongea na malunde 1 blog.
Ng’wamba Susani, mtoto wa Marehemu (Habi Lupigila) anasema serikali
imemkumbushia kifo cha mama yake mzazi wakati huo fedha waliyolipwa kwa ajili
ya fidia haitoshelezi.
Naye John Ndulu Lupigila ambaye ni msimamizi wa wana Ukoo anasema tukio hilo ni sehemu ya maumivu kwa wana ukoo sababu marehemu alifariki tangu mwaka 1975.
Anasema wana ukoo wamechangishana fedha ili kuweza kufidia gharama za kuhamisha kaburi kutokana na fedha walizolipwa na serikali kutokidhi mahitaji ya zoezi hilo.
Goromondo Isamula mkazi wa Nkindwabiye anasema marehemu alikuwa ameolewa na Madako Amva, alifariki muda mrefu na kaburi hilo lilikuwa kwenye zizi ambapo familia ilijengelea baada ya barabara kupita.
Anaongeza
kuwa kaburi hilo lilikuwa njiani, lilikuwa hatari kwa sababu magari yangeweza
kugongana na wao kama wananchi wamefurahi kaburi hilo kuondolewa njia sababu
barabara imeonekana.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Nkindwabiye Safari Ng’habi Himbo ameishukuru
serikali pamoja na wananchi kwa mwitiko wa kushiriki zoezi la kuhamisha kaburi
lililokuwa kikwazo katikati ya barabara hiyo.
‘’Niwashukuru
ndugu kwa kukubwali wito wa serikali kwa kuondoa kaburi hili lililokuwa adha
kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na magari, ilikuwa ni shida magari yalikuwa
yanasababisha ajali katika eneo hili’’ anasema Safari.
Anaeleza
kuwa aliishawishi serikali pamoja na ndugu ili waweze kukubaliana na hatimaye
kulitoa kaburi, ‘’nashukuru Serikali upande wa TARURA, wananchi sambamba na
ndugu tumekubaliana kutoa mwili kuoka hapa Nkindwabiye kwenda kata ya
Matongo’’. anasema.
No comments
Post a Comment