Halmashauri ya Mafinga mji yapongezwa kupata hati safi miaka sita mfululizo
Halmashauri ya Mafinga Mji imepogezwa
kwa kupata hati safi
miaka sita mfululizo kutoka kwa mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) ambayo imeendelea
kuupatia heshima mkoa wa Iringa.
Pongezi hizo zimetolewa na mkuu wa
mkoa wa Iringa Queen Sendiga wakati wa baraza kupitia hoja za CAG , ambapo
alilipongeza baraza la halmashauri ya Mafinga Mji kwa
kufanya kazi vizuri na ndio wamekuwa mfano kwa halmashauri nyingine za mkoa wa Iringa
kuwa na uongozi bora na wenye ushirikiano
Sendiga alisema kuwa hati hiyo safi imetokana na kufanya kazi
kwa ushirikiano hivyo
kupelekea halmashauri hiyo kupata hati hiyo.
Aidha aliwataka watumishi wa
halmashauri ya Mafinga Mji kuendelea kufanya kazi kwa kujituma kulingana na
eneo ambalo analifanyia kazi.
Pamoja na hayo Sendiga alimuagiza
mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji kuwachukulia hatua za kisheria kwa
watumishi ambao wamekuwa wazembe kazini na kusababisha hoja za CAG.
“haiwezekani kila wakati mtumishi
anakuwa anasababisha hoja za CAG na hakuchukuliwi hatua yoyote na anaendelea
kufanya kazi hapo hapo bila kuwajibishwa”.Sendiga
Hata hivyo alisema zilipatikana hoja
30 za mkaguzi wa hesabu
za Serikali (CAG) ambapo jumla ya hoja kumi na tatu (13) zimefanyiwa kazi na hoja
kumi na saba (17) bado hazijafanyiwa kazi hivyo amegiza hoja hizo zifanyiwe
kazi haraka iwezekavyo.
“haiwezekani watumishi wawili ndio
wachukuliwe hatua za kisheria wakati wengine wakiwa wameacha bila kuchuliwa
hatua hivyo amemugiza mkurugenzi kuwachulia hatua za kisheria watumishi”.Alisema
Sendiga
Sendiga alisema kuwa baadhi ya
watumishi ambao wanahusika
kukusanya mapato wamekuwa sio waamifu kwa kuwa wamekuwa wanazima mashine za kukusanyia
mapato.
“Haiwezekani mashine inazimwa kwa
zaidi ya siku 1000
haifanyi kazi na viongozi mpo hapo haiwezekani kabisa nakwambia mkurugenzi wachukuliwe
hatua kali watumishi wanaosababisha kupotea kwa mapato ya halmashauri”alisema
Sendiga
Alimazia kwa kusema kuwa matumizi
yoyote ya fedha za halmashauri lazima yafuate utaratibu na kanuni zake
ili kuhakikisha hazitokei hoja nyingine kwa CAG.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa Wanafanya vizuri kwenye ukusanyaji
mapato, ushirikiano mzuri,wanatoa mikopo, wanafanya vizuri kwenye uchumi
kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano.
Mtambule alisema kuwa mkurugenzi wa
halmashauri ya Mafinga Mji amekuwa kiunganishi kikubwa baina ya wakuu idara na wafanyakazi
wengine wa halmashauri kuwa kitu kimoja katika kufanya kazi.
Alisema kuwa ukatilii wa kijinsia
bado upo wilaya ya
Mufindi lakini wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara ili kuhakikisha wananchi wanajua
madhara ya ukatili wa kijinsia na kupinga vitendo vyote ya ukatili.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya
Mafinga Mji Happiness
Laizer alisema kuwa wameyapokea maagizo yote ya mkuu wa mkoa juu ya hoja za CAG
na watayafanyia kazi ili kuhakikisha hawapati hoja nyingine mpya huku
wakijitahidi kuzijibu na kuzimaliza hoja zote za CAG.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga akiwa na mwenyekiti na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Mji wakati wa baraza la kupitia hoja za CAGMkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji Happiness Laizer akiongea wakati wa baraza la kupitia hoja za CAG
No comments
Post a Comment