Kifo cha Maradona wauguzi Kortini
Madaktari
na Wauguzi wanane waliokuwa wakihusika na uangalizi wa nguli wa soka Diego
Maradona watafikishwa mahakamani wakishtakiwa kwa makosa ya uzembe katika kifo
cha mwanasoka huyo maarufu Duniani.
Jaji
mmoja ameamuru kusikilizwa kwa kesi ya mauaji bila kukusudia baada ya jopo la
madaktari kubaini matibabu ya Maradona yalijaa ‘mapungufu na dosari’.
Maradona
alifariki mnamo Novemba 2020 kwa mshtuko wa moyo huko Buenos Aires, akiwa na
miaka 60 licha ya kuwa alikuwa akipata nafuu nyumbani kutokana na upasuaji wa
kuganda kwa damu kwenye ubongo mapema mwezi huo.
Siku
chache baada ya kifo chake waendesha mashtaka wa Argentina walianzisha
uchunguzi kuhusu madaktari na wauguzi waliohusika katika uangalizi wake.
Mwaka
jana, jopo la wataalam 20 walioteuliwa kuchunguza kifo chake liligundua timu ya
matibabu ya Maradona ilifanya “njia isiyofaa, yenye upungufu na ya kutojali”.
No comments
Post a Comment