Kufutwa ada kwa wanafunzi kidato cha tano na sita kwawaibua UWT Njombe
Pendekezo la
kufutwa ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita yaliyosomwa Bungeni na Waziri
wa Fedha yamepokelewa kwa shangwe kubwa Umoja wa Wanawake wa Chama cha
Mapinduzi(UWT)Mkoa wa Njombe.
Kupitia kwa
Mwenyekiti wa Mkoa huo Scholastika Kevela umoja huo umetoa pongezi hizo baada
ya Waziri Nchemba kusoma mependekezo ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2022-2023
ambayo pamoja na mambo mengine imependekeza kufutwa kwa ada hiyo kwa wanafunzi
wa vidato hivyo.
Hatua hiyo
muendelezo wa mambo mbalimbali makubwa yanayoendelea kufanywa chini ya uongozi
wa Rais Samia Suluhu Hassan tangu aapishwe kwa mujibu wa katiba kuwa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zaidi ya Mwaka mmoja uliopita.
Mama Kevela
amesisitiza kwamba UWT Mkoa wa Njombe hauna chochote cha kumpa Rais Samia zaidi
ya kumshukuru kwa hatua hiyo ambayo inakwenda kuyafuta kabisa machozi ya
watazania wengi hususani wanyonge wenye vipato vya chini.
” UWT Mkoa wa
Njombe tunazidi na tutazidi kuendelea kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa
hatua nyingi anazozizifanya kuwapunguzia mzigo watanzania , amefuta vilio vya
masikini wengi waliokuwa wahihi kutafuta hela kuwalipia watoto wao ada” alisema
Kevela
Ameongeza kuwa baada
ya hatua ya aliyekuwa Rais mstaafu wa awamu ya Tano marehemu Dk John Magufuli
kufuta ada kwa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, Rais Samia ‘
ameupiga mwingi’ kwa pendekezo lake la kufuta ada kwa kidato cha tano na sita
Awali akisoma
mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya Mwaka 2022-2023 Bungeni Waziri wa Fedha Dk
Mwigulu Nchemba alisema katika utekelezaji wa bajeti hiyo, Rais Samia alitoa
mapendekezo ya kuondolewa kwa ada hiyo hatua ambayo kila mtanzani ameipokea kwa
furaha.
” Kwa hilo hakuna
ubishi, ni hapa juzi tu katoka kuwaondolea wafanyabiashara mzigo wa malimbikizo
ya Kodi pamoja na ushuhuru mbalimbali wa zaidi ya miaka mitano iliyopita,
alipandisha kima cha mishahara katika sekta ya umma nchini ili alilolifanya leo
ni zaidi ya upendo kwa wananchi wake” alisisitiza Kevela
Alisema hatua hiyo
ameonyesha kulijali Taifa analoliongoza kwani amewatua mzigo mzigo mzito
wananchi wake hali iliyopelekea elimu nchini kuwa bure kuanzia elimu ya awali
hadi kidato cha sita jambo ambalo halijawahi kutokea tangia uhuru.
“Watanzania watake
nini zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Njombe
nikiwa Mwenyekiti wao UWT niwatake wanawake wenzangu waliopo kila kona ya
Tanzania kujitokeza na kuzitangaza kazi nzuri anazozifanya Rais Samia ”
alisisitiza Scholastika Kevela
Mwenyekiti wa
umoja huo pia aliwataka wanaume wote nchini kulichukulia suala hilo kwa uzito
mkubwa kwani kitendo alichokifanya Rais kuondoa ada hiyo kinawapunguzia mzigo
wa kusomesha watoto waliokuwa nao.
Pamoja na hayo alisema
watanzania wote wamelipokea suala hilo kwa mikono miwili na zaidi ana amino
kuwa wakati wote wataendelea kumuunga mkono huku akiwataka kumuombea Dua njema
kwa Mungu apate kuwa na afya njema wakati wote ili azidi kuwatumikia.
No comments
Post a Comment