Makada 19 wa Chadema waachiwa huru Mwanza
Viongozi
na wanachama 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa
wakikabiliwa na shtaka la kufanya fujo kwenye mkusanyiko wa kidini katika
Kanisa Katoliki Parokia ya Kawekamo jijini Mwanza wameachiwa huru.
Washtakiwa
hao wameachiwa huru leo Juni Mosi, 2022 na Hakimu Mkazi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Bonaventure Lema baada ya upande wa
mashtaka kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo namba
77/2021.
Kwa
mara ya kwanza makada hao walifikishwa mahakamani Agosti 19, 2021 wakidaiwa
kutenda kosa hilo Agosti 15, 2021 baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili katika
Kanisa Katoliki parokia ya Kawekamo wakiwa
wamevaa sare za chama chao na fulana nyekundu zilizoandikwa Katiba Mpya.
Walioachiwa
huru ni pamoja na Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria,
Zakaria Obadi, Deus Shinengo, mang’ombe Oswald, Kelvin John, Farida Gilala,
John Nyamhanga, Emmanuel Mtani na Frank Nyamuga.
Wengine
ni Msafiri Nteminyanda, Musa Kimweri, Gadson Jacob, Elieza Mkungu, Dionise
Edward, Michael Christian, Leah Joseph, James Mayala, Yasinta Wachelele na
Eudia Frank. Washtakiwa wote walikuwa wanawakilishwa na Wakili Erick Muta.
Akisoma
hati ya mashtaka wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani kwa mara ya
kwanza Agosti 19, 2021, Wakili wa Serikali, Bisela Bantulaki alidai mbele ya
Hakimu Mkazi Emmanuel Lukumay kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Agosti 15,
2021 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kawekamo Wilaya ya Ilemela jijini
Mwanza.
Wakili
Bantulaki alidai kwa pamoja, washtakiwa ambao wote walikana mashtaka dhidi yao
walifanya fujo wakati ibada ya matoleo ikiendelea.
Akizungumza mara baada ya wanachama hao kuachiwa huru wakili
Erick mutta amesema kesi hiyo imeondolewa
kwa hati ya kufutiwa mashtaka iliyoletwa na jamhuri na wao wamepokea uamuzi huo mahakamani hapo na
kusema kwa sasa watuhumiwa wote 19 wapo huru na wanaruhusiwa kuendelea na
shughuli zao .
kwa upande wake mwenyekiti wa BAVICHA taifa, John Pambalu,
amempongeza mwanasheria Erick Mutta, kwa
kazi kubwa aliyoifanya mahakamani
kuwawakilisha niwanachama waliokuwa
wanakabiliwa na kesi hiyo.
Pambalu amesema BAVICHA inatoa wito kwa Jamhuri, kuendelea
kufuta kesi za kisiasa ambazo zinawakabili viongozi na wanachama wa chadema katika uchaguzi wa mwaka 2020,baada na kabla
ya uchaguzi huo.
“zipo kesi nyingi kama kesi ya mauaji inayomkabili george sanga na wenzake kule njombe, ipo kesi
ya aliyekuwa diwani wetu kule Mpanda, na
kesi nyingine nyingi ambazo bado zinawakabili wanachama wetu” amesema Pambalu
“tunataka jamhuri iweze kuziondoa na waliokwisha kuhukumiwa
waachiwe huru ili waweze kuendelea na
maisha yao “
Aidha amesema kazi
yao kama BAVICHA ni kuendelea kuwatia moyo watuhumiwa, mahabusu pamoja na
wafungwa ambao wapo mahahamani kwa
sababu za kisiasa
“tunatamani kuanza upya kwa kuachilia na kufuta kesi zote za kisiasa”
Washtakiwa
wote walikuwa nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya mdhamini aliyesaini
hati ya dhamana ya Sh1 milioni, barua ya utambulisho kutoka ofisi ya Serikali
ya Mtaa na nakala ya kitambulisho cha mpigakura au cha Taifa.
No comments
Post a Comment