Marufuku kusafirisha mazao bila kuwa na kibali:Bashe
Waziri wa Kilimo, Hussein
Bashe amevitaja vibali stshiki ambavyo anatakiwa kuwa navyo mfanyabiashara ili
aruhusiwe kusafirisha mazao.

Bashe amesema vibali
hivyo ni pamoja na kibali cha kusafirisha mazao nje ya nchi na cha usafi wa
mazao (Phytosanitary) huku akiwataka wafanyabiashara wa
mazao kutafuta vibali hivyo kabla ya kuanza kuyanunua kwa wakulima
Bashe ametoa agizo hilo
kwa wafanyabiashara katika kikao chake na Vyombo vya Habari kilicholenga kutoa
suluhisho kwa malori yaliyokwama mipakani hususan mpaka wa Tanzania na
Kenya- Namanga ambapo kuna malori zaidi ya 40 yamekwama yakiwa yamebeba mazao
mbalimbali.
Bashe alisema, imekuwa ni
tabia kwa wafanyabiashara hao kuanza kukusanya mazao ya wakulima bila ya kuwa
na vibali vya kuyasafirisha na kisha kuanza kutafuta vibali wakifika mpakani.
Alisema, tukio hilo ni
mara ya pili kutokea ambapo kwa awali lilipotokea serikali iliwasamehe na
kuruhusu kusafirisha mazao na tukio la sasa pia inawasamehe wasafirishe mazao
lakini amewakanya kuwa haitokuwa na msamaha tena.
“Hili tukio la sasa hivi
ni mara ya pili linajitokeza ambapo awali walisamehewa na kwa kuwa serikali
haitaki kuwaumiza wakulima kwa kuzuia kusafirishwa kwa mazao hayo na hili la
sasa tunawasamehe, ila iwe ndiyo mwanzo na mwisho wakirudia tena mazao yao yote
tutachukua.” alisema Bashe.
Alisema vibali vinatolewa
bure kwa njia ya mfumo ATMIS mtandaoni hivyo hakuna sababu ya wafanyabiashara
hao kukwepa kutafuta huku akiwataka pia kuwa na vibari vya tathmini ya mazao.
Alisema faida ya kuwa na
vibali hivyo ni kuwezesha kupatikana kwa takwimu sahihi kuhusu kiwango cha
mazao kinachosafirishwa nje ya nchi na nchi yanapokwenda ili kuondoa mwanya wa
watu wengine kupeleka mazao yasiyokuwa na kiwango kwenye nchi hizo kisha
kusingizia kuwa yametoka Tanzania.
Kutokana hali hiyo Bashe
alisema kuwa serikali haitosita kuyachukua mazao yatakayokamatwa tena
siku nyingine yakisafirishwa bila vibali
No comments
Post a Comment