Mhariri mtendaji mstaafu wa uhuru/mzalendo mzee Mufungo afariki dunia
Mahariri Mtendaji mstaafu wa Magazeti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Uhuru na Mzalendo Mzee Josiah Mufungo, amefariki Dunia.
Taarifa zimesema Mufungo amefariki usiku wa kuamkia leo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Lugalo, Dar es Salaam.
Wakati akiwa Mhariri Mtendaji, magazeti ya Uhuru na Mzalendo yalikuwa yanachapishwa na Kampuni ya Uhuru Publications Limited, magazeti hayo sasa yanachapishwa na UMG ambayo inasimamia vyombo vya Habari vya CCM ikiwemo Uhuru fm.
Msimamizi Mkuu wa Blog hii kwa niamba ya timu nzima, anatoa pole za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo.

No comments
Post a Comment