Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemkuta na kesi ya kujibu, Mhasibu Mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu), Sospeter Omollo.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi, Juni 2, 2022 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi iwapo mshtakiwa ana kesi ya kujibu au laa.

Omollo anakabiliwa na mashtaka 47 yakiwemo ya kughushi nyaraka na kufanya ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh410 milioni, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 5/ 2021.