Header Ads

Header ADS

Polisi Dar yamsaka mtuhumiwa wa mauaji ya raia wa China



Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wanamsaka raia wa China Zheng Lingyao (42), mkazi wa Dar es salaam anayetuhumiwa kumuua raia mwenzake Fu Nannan, (26).

Muliro amesema tukio hilo limetokea Juni 11 majira ya saa 5:45 usiku katika mtaa wa Kalenga, Ilala jijini Dar es salaam, eneo alilokuwa akiishi marehemu.

“Mtuhumiwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni mwanamke mmoja Nie Mnqin naye ni raia wa China na baada ya kumjeruhi mwanamke huyo alimfyatulia risasi Fu Nannan,” alisema Muliro

Mwanamke huyo majeruhi Mnqin, anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili na uchunguzi wa awali umebaini tukio hilo linahusisha mambo ya kimapenzi. 

No comments

Powered by Blogger.