Uhamiaji watakiwa kuimarisha usalama Loliondo
Idara
ya Uhamiaji nchini imetakiwa kuhakikisha inasimamia uingiaji na utokaji wa
wageni katika mipaka ya nchi kwa kufuata sheria.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni akiwa Loliondo,
Ngorongoro Mkoani Arusha wakati akikagua maendeleo ya zoezi la uwekaji wa alama
za mipaka katika eneo la pori tengefu la eneo hilo.
Amesema
Serikali itafanya uhakiki wa kina ili kubaini uendeshaji wa asasi za kiraia
nchini, ikiwemo namna wanavyofanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na kwamba
zitakazokiuka zitachukuliwa hatua za kisheria.
Waziri
Masauni ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya zoezi huku akiwataka
wahusika kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kwa wakati.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Mwl. Raymond Mangwala amesema
wamepokea maelekezo ya waziri na kwamba watahakikisha hali ya usalama wa
wananchi na mali zao inaendelea kuimarishwa.
Mwl.
Mangwala ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela
alimueleza Waziri Masauni kuwa na kuwa zoezi hilo litaendelea kwa hali ya amani
na utulivu katika eneo hilo la Wilaya ya Ngorongoro.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akiwana baadhi ya Viongozi na Askari Wilayani Ngorongoro, alipotembelea eneo hilo kuangalia maendeleo ya zoezi la uwekaji alama kwenye mipaka ya pori tengefu la Loliondo lililopo Mkoani Arusha.
No comments
Post a Comment