Umoja wa wabunge wanawake wa EALA wakutana Arusha kubadilishana uzoefu
Umoja wa wabunge wanawake wa bunge la Jumuiya
ya Afrika Mashariki pamoja na viongozi kutoka Afrika wamekutana jijini Arusha
katika mkutano wa kimataifa wa wabunge wa kikanda ili kubadilishana uzoefu na
mawazo haswa wa wabunge wanasiasa.
Mbunge wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wanawake kutoka nchi za Afrika katika mkutano ulionza jijini Arusha.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu ulioandaliwa na bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Idea International na kufanyika Arusha Mwakilishi wa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ni mbunge wa bunge hilo Anastazia Wambura alisema ni vyema wanawake wakawa mstari mbele katika kuwania nafasi ya uongozi wa kisiasa kutokana na eneo ambalo maamuzi hufanyika.
No comments
Post a Comment