Wafanyakazi sekta ya Afya waandamana
Wafanyakazi wa sekta afya Zimbabwe, wameanza
mgomo kupinga masharti ya malipo kutokana na mzozo mpya wa kifedha nchini humo
kwa kufikisha ujumbe wao kwa serikali ulio katika mabango nje ya ofisi za
Baraza la Huduma za Afya katika moja ya hospitali kubwa nchini humo.
Wamesema, mpango huo mpya unaotokana na
kuporomoka kwa uchumi unawapa ukakasi na kwamba wamekuwa wakishuka kiufanisi,
huku Askari wa kutuliza ghasia waliwekwa kwenye uwanja wa hospitali hiyo,
kitendo kilichosababisha wagonjwa kukosa tiba.
“Wafanyakazi wa afya wanalipwa ujira mdogo,
Wanajitahidi kujikimu na tuna mahitaji mengi sasa kwa namna hii haifai
tunashuka kiutendaji kitu kitakacholeta madhara,” alisema muandamanaji Kiongozi
wa Muungano wa Sekta ya Afya, Tapiwanashe Kusotera.
Wanasema wao kama Wauguzi nchini Zimbabwe
wanapata dola za Zimbabwe 18,000 kwa mwezi, ambazo ni sawa na takriban dola 55
(euro 52) huku Walimu wakipata takriban $75 kwa mwezi.
“Bodi yetu ya Huduma za Afya ambayo ni mwajiri
wetu na Wizara ya Afya wamekataa kabisa kuzungumza na wafanyakazi hao,” alisema
Mkuu wa Chama cha Wauguzi nchini, Enock Dongo.
Serikali, juma lililopita ilisema kwamba
itaongeza mishahara maradufu ya watumishi wote wa umma, lakini Dongo alisema
hakuna ofa rasmi iliyotolewa mpaka sasa na Juni 20, 2022 Walimu walitangulia
kuitisha mgomo wa siku tano, kulingana na taarifa ya chama cha walimu.
“Hatuwezi kuendelea kuwa aibu kwa jamii yetu
kwa sababu ya umaskini ambao serikali inauchukulia kuwa sehemu ya maisha yetu
ya kufanya kazi,” iliandika.
Uchumi wa Zimbabwe uko katika mgogoro mkubwa,
ikiwa ni pamoja na kujiondoa kwa wafadhili wa kimataifa kwa sababu ya madeni
yasiyo endelevu.
Mfumuko wa bei ulifikia 131% mwezi Mei, na
kufufua kumbukumbu za mfumuko wa bei zaidi ya muongo mmoja uliopita. Bei
zilikuwa zikidorora na benki kuu ilitoa noti ya dola trilioni 100 mwaka 2008,
ambayo imekuwa bidhaa ya ushuru.
Uvamizi wa Ukraine umesababisha hali kuwa mbaya
zaidi, kwani Urusi ndiyo msambazaji mkuu wa ngano na kemikali zinazotumika
katika kilimo cha Zimbabwe.
No comments
Post a Comment