Bashungwa atoa miezi mitatu kwa wakuu wa mikoa yote nchini kukamilisha miundombinu ya shule mpya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ametoa miezi mitatu kwa wakuu wa mikoa yote nchini kukamilisha miundombinu ya shule mpya zinazojengwa kupitia Mpango wa Kuboresha Elimu ya Sekondari(SEQUIP).
Programu hiyo inajenga shule mpya 214 katika kata za majimbo yote nchini ambazo hazina shule za sekondari au ambazo zinafunzi ambapo kila kata imepelekewa Sh milioni 470 huku ikipanga kutoa Sh milioni 130 kwa ajili ya miundombinu ya shule hizo
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa shule mbili za sekondari wilayani Kiteto, Bashungwa alisema wakuu wa mikoa wanapaswa kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo na kusisitiza kuwa Serikali haitatoa fedha zingine.
" Wakuu wa mikoa ama halmashauri muangalie ni namna gani mtakamilisha maeneo ambayo hayajakamilika, mahali pengine ndani ya nchi tumepeleka shilingi milioni 470 miondombinu yote imekamilika na imeanza kutoa huduma kwa watoto
" Nisisitize hatutaleta fedha ya ziada ya shilingi milioni 470 ambazo zimeletwa, hivyo wakuu wa mikoa wote nchini mfuatilie na mhakikishe miradi ya ujenzi wa shule mpya ambayo Serikali imepeleka muikamilishe ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa hadi mwishoni mwa Okotoba."
Bashungwa Pia amewaelekza wakuu wa mikoa kuhakikisha ifikapo Januari 2023 watoto wanaaza kusoma katika shule hizo mpya.
Kuhusu shule za sekondari zilizojengwa katika Kata ya Matui na Namelock, Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere kutumia vyombo vyake kufanya ukaguzi wa fedha zilizotumika katika shule hizo.
" Namemuelekeza Mkuu wa Mkoa Mzee na timu yako hebu jiridhishe na gharama halisi ambayo imetimika mahali hapa, kiasi ambacho mmekiomba hakitatoka Serikali kuu."
No comments
Post a Comment