Kesi ya Manara Vs Rais wa TFF yaanza kuunguruma
Mashahidi waanza kutoa ushahidi wa
tukio la Msemaji wa Young Africans Haji Manara dhidi ya Rais wa Shirikisho la
soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.
Ilitokea sintofahamu Julai 2 wakati wa
fainali ya kombe la FA iliyoikutanisha Young Africans na Coastal Union katika
uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha ilionekana wawili hao wakizozana
katika video iliyosambaa mitandaoni huku watu wakimtuliza Manara.
Julai 3 Sekretarieti ya TFF ilifungua
shauri mbele ya kamati ya maadili dhidi ya Manara kutokana na vitendo vya
ukiukaji wa maadili.
Tayari kesi huyo imeishaanza kuunguruma
na mashahidi wameanza kutoa ushahidi mbele ya kamati hiyo.
Mmoja wa mashahidi alipotafutwa
alikaririwa juu ya kushangazwa na namna mzozo huo jinsi ulivyoibuka.
Licha ya Manara kukutana na Karia na
kuomba msamaha na kuomba hadharani akikiri kukosea kamati imeendelea na kesi
hiyo.
No comments
Post a Comment