Makamba aipongeza bodi ya wakurugenzi TPDC kwa umahiri
Waziri wa Nishati January Makamba
amesema uendeshaji umahiri na umadhubuti wa uongozi wa shirika la TPDC, ni
jambo ambalo serikali unalipa uzito wa hali ya juu.
Makamba ameyasema hayo wakati akizindua
bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo jijini Arusha na kueleza kwamba uteuzi wa
bodi hiyo unaakisi dira na malengo mapya ya serikali kwa shirika hilo kuelekea
katika mafuta na gesi.
Amesema bodi hiyo chini ya Mwenyekiti wake balozi Ombeni Sefue inakidhi nafasi ya TPDC katika maendeleo ya nchi, Dira na mwelekeo mpya wa TPDC katika uchumi mpya wa gesi na maendeleo ya mafuta nchini kwa ujumla.
"Dhamira yetu ni kuona shirika
hili linatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na sio katika mapato tu
bali uendeshaji wa rasilimali watu katika tasnia hii lakini pia ushiriki wa
nchi katika miradi mikubwa ya kimkakati ya mafuta na Gesi" ,alisema
Makamba.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo
ya TPDC Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni katibu mkuu Kiongozi mstaafu amesema
wao kama bodi kazi yao ni kwenda kuchangamsha na kuhakikisha kila kitu kinaenda
inavyotakiwa na sekta hii ili taifa liweze kunufaika na rasilimali zake za
mafuta na Gesi tulizopewa na Mungu.
Awali Mkurugenzi wa Shirika la mafuta
na Gesi nchi muhandisi James Maragio amesema kuwa miradi ya mafuta na Gesi
itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto za wananchi.
Alisema kuwa wana miradi mikubwa
ikiwemo mradi wa bilion 40 ikiwemo mradi wa kujenga bomba la mafuta kutoka
hoima Uganda ambao umeonyesha mafanikio pia kuna maradi wa kutafuta mafuta
katika bonde la ufa ambao upo kwenye Mchakato.
No comments
Post a Comment