Ubakaji wa watoto chanzo cha Fistula:Rais Samia
Rais Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la
Fistula kwa watoto wa mwaka 4 hadi 12 linasababishwa na ubakaji.
Mhe. Samia ameyasema hayo alipotembelea
hospitali ya CCBRT na kukagua wodi ya wanawake wenye matatizo ya Fistula.
Amesema inakadiriwa wanawake 12000 Hadi 18000
wana tatizo la fistula huku watoto wakikadiriwa kuwa na miała 4 hadi 12
wakiwemo katika orodha hiyo.
“Ndugu zangu watanzania, Tatizo hili la
ubakaji ambalo kwa kiasi kikubwa tunalifumbia macho kwenye jamii hatuwapeleki
kwenye combo via Sheria tunakosea.”
Ameongeza, “kwa hiyo niwaombe sana ndugu
zangu tupunguza sana idadi hiyo ya wanawake wanaoishi na fistula nchini kwa
kuepuka yanayoweza kuepukika ambayo ni Ndoa za utotoni, ubakaji, mimba za
utotoni na mila potofu,”
Rais Samia alikua mgeni Rasmi katika uzinduzi
wa Jengo jipya la mama na mtoto hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam, Leo
Julai 5, 2022.

No comments
Post a Comment