Wanahabari nchini wajengewa uwezo wa kuripoti habari kuhusu haki za binadamu
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amewataka wanahabari kuendelea
kufanya kazi kwa bidii na weledi zikiwemo za utetezi wa Haki za binadamu ili
kuongeza tija katika kuwahabarisha wananchi taarifa zilizojitokeza na
zitakazojitokeza.
Msando amesema hayo leo Mkoani Morogoro
wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari kuhusu namna Bora ya
kutoa habari ambayo yameratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Tanzania -THRDC
Aidha Mkuu huyo Wilaya amewataka wanahabari
kujitahidi kuwa watetezi wa Haki za Binadamu bila ya kuwa mashabiki wa kuegemea
upande mmoja ili kuepukana na changanoto mbalimbali.
Amesema waandishi wa habari wanapozungumza
Masuala ya Haki za Binadamu wasiwe wazito kwa kutozitoa badala yake waangalie
mzani na ukweli katika kuhabarisha umma Juu tukio wanalotaka kuliripoti.
Naye Mhe jaji Mstaafu Robert Makaramba
amewasilisha mada ya wanahabari namna ya kuandika na kuripoti habari za kwenye
mahakama kuwa ni vyema wakaepuka kutoa taarifa ambazo hazijatolewa mahakamani
ili kuepusha sintofahamu kwenye jamii.
Awali akizungumza Wakili Kutoka Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu -THRDC Leopold Mosha amesema Mafunzo hayo
yamelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika ma kuripoti
taarifa zinazohusiana na haki za Binadamu.
Wakili Mosha amesema kuwa Moja ya majukumu ya
Asasi za Kiraia ni kufanya uchechemuzi wa kujua na kupata ufahamu wa Masuala
mbalimbali yanayohusu Haki za Binadamu.
Kwa Upande wake Afisa Uchechemuzi -THRDC Nuru
Maro wakati aliwasilisha mada ya Umuhimu wa waandishi wa habari Katika kufanya
uchechemuzi kuwa ni Pamoja na kufahamu Chanzo,Ushahidi,kujua Watu wengine
wanavyofanya kazi Hilo Eneo husika.
“Ili kuwe na mabadiliko lazima umma uelewe
hivyo ni vyema wanahabari mukaonyesha Umuhimu Katika kutoa elimu kuhusiana na
Masuala ya Haki za Binadamu Pindi munapoona Kuna ukiukwaji”amesema Nuru
Hata katika mafunzo hayo ambayo ambayo yameanza Leo na yanamalizika siku ya kesho July 13 wanahabari wamesisitizwa kutumia fursa hiyo kujiongezea maarifa katika ufanyaji wao wa kazi.
Mhe jaji Mstaafu Robert Makaramba akiwasilisha mada ya wanahari namna ya kuandika na kuripoti habari za kwenye mahakama katika mafunzo kwa wanahabari kuhusu namna Bora ya kuandika habari hasa za Haki za Binadamu ambayo imefanyika Leo Mkoani Morogoro.
Wakili Kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu -THRDC Leopold Mosha akieleza dhumuni la Mtandao Huo kuandaa Mafunzo hayo ambayo yamefanyika Leo Mkoani Morogoro
Afisa Uchechemuzi -THRDC Nuru Maro wakati akiwasilisha mada namna ya Umuhimu wa waandishi wa habari na katika kufanya uchechemuzi.
No comments
Post a Comment