Wezi wa Vyuma na Minyororo barabarani kukiona chamtemakumi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ameshirikiana na Maelfu ya Wakazi wa Jiji Hilo kwenye zoezi la Usafi wa pamoja kwenye Barabara kuu za Mkoa huo ambapo kila Mkuu wa Wilaya ameongoza Usafi kwenye eneo lake.
Katika zoezi Hilo RC Makalla pia amepokea msaada wa Vifaa mbalimbali vya Usafi kutoka Kampuni TCC Sigara iliyounga mkono Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM kwa kutoa Toroli 50, Pipa 470 za kuhifadhi taka, Reki 50 na Fagio 50 ambapo wameahidi kuendelea kutoa Vifaa kila Baada ya miezi miwili.
Akizungumza na Wananchi na Wadau waliojitokeza kushiriki usafi,RC Makalla amesema katika awamu pili ya Kampeni ya Usafi Mkoa umejipanga kuboresha na kupendezesha mandhari ya Barabara kuu kwa kuhakikisha upandaji miti, uwekaji bustani za watu kupumzika, mifumo ya umwagiliaji na utengenezaji wa Fountains.
Aidha RC Makalla amesema Mkoa pia umeweka mkakati endelevu wa kudhibiti Wizi wa vyuma na minyororo kwa kufunga Camera Barabarani ili kubainii Wezi.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Halmashauri kushirikiana na *Shirikisho la bodaboda* kwenye Ujenzi wa *Vituo vya kisasa vya Bodaboda* ambavyo vimesajiliwa na kuratibiwa vizuri ambapo licha ya *kupendezesha mandhari pia itasaidia kudhibiti uhalifu.*
Hata hivyo *RC Makalla* amepongeza na kuishukuru Kampuni ya *TCC Sigara* kwa kushirikiana na Mkoa bega kwa bega kwenye Kampeni ya *SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM.*
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa Kampuni ya TCC Sigara *Ndg.Paul Makanza* amesema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Mkuu wa Mkoa kuhakikisha Dar es salaam inakuwa safi.
No comments
Post a Comment