Jeshi la ukraine lashambulia madaraja ya mto Dnieper.
Jeshi la Ukraine limedai kuyashambulia madaraja ya kimkakati katika mto Dnieper uliopo kwenye eneo linalodhibitiwa na Urusi.
Moja ya madaraja hayo hutumiwa kama njia kuu ya usambazaji kati ya jiji la Kherson ambalo linakaliwa na Urusi na askari wake. Daraja la Antonivskiy liliharibiwa katika shambulizi la awali, huku vikosi vya Urusi vikipanga kumaliza ukarabati na kulifungua tena Jumatano hii.
Maafisa wa Urusi wamedai kwamba hakuna uharibifu mkubwa wa daraja katika mashambulizi ya hivi karibuni. Ukraine imekuwa ikitumia mizinga ya masafa marefu iliyotolewa na Marekani kujaribu kuizuia Urusi kusonga mbele upande wa mashariki. Vikosi vyake vina matumaini ya kulidhibiti tena jiji la Kherson lenye wakaazi karibu laki tatu kutoka mikononi mwa Urusi.
No comments
Post a Comment