Mahakamani kwa mauaji ya watu 150 .
Kesi ya Dikteta wa zamani wa Guinea, Moussa Dadis Camara, imefunguliwa hi leo mjini Conakry, ikiwa imepita miaka 13 sasa tangu mauaji yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 150 katika mkutano wa kisiasa mjini humo.
Dikteta huyo wa zamani na washtakiwa wengine watano, jana Jumanne Septemba 27, 2022 waliwekwa gerezani na Mahakama ya Rufaa, hatua ambayo ilishutumiwa vikali na mmoja wa mawakili wao, Me Salifou Béavogui.
Salifou Béavogui alisema, “Tulijipanga kumshawishi mwendesha mashitaka sababu walienda kwenye kesi kama sisi tulivyokwenda, na usiku wa kuamkia kesi huwezi kuwaita washitakiwa hakuna aina ya kizuizini lakini kwa bahati mbaya hatukueleweka.”
Naye, Wakili wa mshtakiwa mwingine, Claude Pivi amesema “licha ya ahadi za mara kwa mara chini ya utawala wa rais wa zamani wa Guinea, Alpha Conde waathiriwa na jamaa wamekuwa wakisubiri haki kwa miaka 13 na hatimaye, waliwapeleka wateja wetu gerezani kwa ajili ya ufunguzi wa kesi kesho.”
Septemba 28, 2009 Rais wa Muungano wa Wazazi na Marafiki wa Waathiriwa, Asmaou Diallo alisema “Wakati wote tulikuwa tukimuomba Alpha Condé (Rais wa zamani wa Guinea), akubali na kuwaweka kizuizini hadi wakati ambapo haki itapatikana sasa leo wako katika gereza kuu.”
Washtakiwa wachache, wamezuiliwa kwa miaka mingi na wale ambao walikuwa bado huru walikamatwa hapo jana Jumanne baada ya kuitwa majira ya saa sita mchana na Camara, ambaye alikuwa akiishi uhamishoni nchini Burkina Faso, alirejea Conakry Jumamosi usiku (Septemba 23, 2022), kujibu mashtaka.
No comments
Post a Comment