Header Ads

Header ADS

Mwanafunzi UDSM ,auawa na kikundi cha waalifu

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Wiliam Mkonda amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi wa stashahada ya uandishi wa habari Maria Basso (24).

Maria ambaye alikua mwaka wa pili katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amefariki dunia baada ya watu zaidi ya 10 kuvamia nyumbani kwao.

Kamanda Mkonda amesema tukio hilo limetokea Septemba 14 saa 2:30 usiku maeneo ya Kawe mzimuni, ambapo kikundi cha wahalifu wakiwa na silaha za jadi, walivamia nyumbani kwa Paschal Basso (56). 


Amesema baada ya kuvamia nyumba hiyo yenye vyumba 15, walivunja milango na kupora fedha, simu za mkononi, kujeruhi watu watatu na kumuua mtu mmoja ambaye ndio Maria.

“Tukio walilofanya wahalifu hawa ni baya na linalotakiwa kulaaniwa na kukemewa na Mtanzania yoyote anayechukia uhalifu kwa watu kama hawa ambao hawataki kutumia njia halali za kujitafutia kipato,” amesema Kamanda Mkonda.

“Tunaendelea kuwasisitiza viongozi wa serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika kukabiliana na uhalifu wa aina hii katika maeneo yao,” ameongeza.


No comments

Powered by Blogger.