Header Ads

Header ADS

Ruto aapishwa kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya

 


Msajili Mkuu wa Mahakama Anne Amadi, amemuapisha William Samoei Ruto rasmi Jumanne, Septemba 13 kama Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya mbele ya Jaji Mkuu Martha Koome.

Ruto amekula kiapo hicho katika uwanja wa michezo uliojaa watu Kasarani na kushuhudiwa na zaidi ya wakuu wa nchi mbalimbali wapatao 20.

Ruto mwenye umri wa miaka 55 amekula kiapo kwa kutumia nakala ya katiba ya Kenya, wiki tano baada ya uchaguzi wa Agosti 9, akichukua hatamu za nchi iliyokumbwa na ukame na mzozo wa gharama ya maisha.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikutana na Ruto Ikulu Jumatatu, Septemba 12, alithibitisha kwamba ataheshimu mamlaka yake ya kikatiba ya kukabidhi mamlaka.

“Kama alama mahususi ya demokrasia yetu, kesho, mbele ya Mungu na wananchi wenzangu, nitakabidhi ala za mamlaka kwa Rais wetu mpya katika Kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Moi, Kasarani. Kwa hayo, Utawala wa Nne utafikia kikomo na muda wa Utawala wa Tano utaanza,” Uhuru alisema.

No comments

Powered by Blogger.