Header Ads

Header ADS

Walioambukizwa Ebola wafikia 16 Uganda

 

Serikali ya Uganda imesema jana kuwa watu 16 nchini humo wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola kufikia sasa huku wengine 18 wakishukiwa kuwa na maambukizo ya virusi hivyo hali inayochochea hofu ya kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa huo ambao chanjo yake bado haijapatikana.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, wizara ya afya nchini humo imethibitisha vifo vya watu wanne kutokana na ugonjwa huo huku wengine 17 walioshukiwa kuwa na ugonjwa huo pia wakifariki dunia.

Mripuko huo sasa umeenea katika wilaya tatu zote zikiwa katikati mwa Uganda. Mlipuko wa Ebola ulitangazwa wiki iliyopita kutokea katika wilaya ya Mubende nchini humo. Maambukizi ya ugonjwa huo mara nyingi husababisha homa kali na kutokwa na damu ndani.


No comments

Powered by Blogger.