Waziri Mabula awataka wafanyakazi wa wizara ya ardhi wasifanye kazi kimazoea
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akizungumza katika kikao kazi cha Makamishna Wasaidizi wa ardhi wa mikoa leo Septemba 6,2022 katika ofisi za NHC Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akizungumza katika kikao kazi cha Makamishna Wasaidizi wa ardhi wa mikoa leo Septemba 6,2022 katika ofisi za NHC Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi cha Makamishna Wasaidizi wa ardhi wa mikoa leo Septemba 6,2022 katika ofisi za NHC Jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amemuelekeza Katibu wa Wizara hiyo kuhakikisha anaanza kuchukua hatua mara moja kwa Makamishna wasaidizi wa ardhi wale walioshindwa kukidhi matarajio pamoja na wasaidizi wao.
Ameyasema hayo leo Septemba 6,2022 Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha Makamishna wasaidizi wa ardhi wa mikoa ambapo amesema wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea, wanaogopana, wanalindana na hivyo kuathiri utendaji wa kazi.
Amesema pamoja na hatua za kinidhamu ambazo zimechukuliwa kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kuwaachisha kazi kwa Mikoa ya Mbeya (3) na Dodoma (4), ameagiza hatua zichukuliwe kwa Mikoa mingine.
“Kwa mashauri ya kinidhamu ambayo yanaendelea, naelekeza yakamilishwe haraka. Mikoa ambayo tunakamilisha taratibu za kinidhamu kwa watumishi siku za hivi karibuni ni Mbeya, Dar es Saaam, Mwanza na Arusha na Lindi”. Amesema Waziri Mabula.
Aidha Dkt.Mabula amesema wamebaini kuwa wapo watumishi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya udanganyifu kwenye zoezi la uthamini wa mali ambapo majina yao wameyapata na watachukua hatua za haraka.
“Siridhishwi kabisa na utendaji wa Mkurugenzi wa TEHAMA. Naelewa Katibu Mkuu analifanyia kazi; naelekeza lifanyiwe kazi kwa haraka na kwa muda mfupi”. Amesema
Pamoja na hayo Dkt.Mabula amesema vituo vya mafuta hivi sasa vinajengwa kila sehemu bila udhibiti na uratibu mbele ya macho ya makamishna wasaidizi wa ardhi kama wasimamizi wa Sekta katika Mikoa yao, hivyo ameagiza likasimamiwe ipasavyo na kwa nguvu zote.
No comments
Post a Comment