Jeshi la polisi mkoani Dodoma lipo katika msako wa kumtafuta Juma Linoga anaedaiwa kumuua mkewe
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, lipo katika msako wa kumtafuta mkazi wa Kata ya Bahi Sokoni, Juma Linoga anayedaiwa kumuua mkewe, Mariam Alex (34), na kuufunika mwili wake kwa mifuko ya saruji.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amesema mauaji hayo yalitokea Oktoba 15, 2022 na mtuhumiwa wa tukio hilo amekimbia huku mwili wa Mariam ukigundulika katika pagale hilo baada Polisi kupata taarifa.
Amesema, “Tuliukuta mwili ukiwa umepigwa na kitu sehemu mbalimbali lakini bado tunafanya uchunguzi kujua chanzo cha mauaji hayo ni nini ili hatua kali zichukuliwe kwa waliohusika na muhusika alikimbia na bado tunamtafuta.”
Akisimulia tukio hilo, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Nkungugu, Pascal Mchela alisema Oktoba 13, 2022 mtoto marehemu Mariam, alisema mtuhumiwa (Juma Linoga), alifika nyumbani kwa mkewe usiku na kumuita bila mafanikio, na baadaye kugundulika tukio la mauaji hayo.Jeshi
No comments
Post a Comment